Sunday, May 10, 2015

Jaalab Enterprises Ltd na Mpango wa kuuza Vifaa vya Maabara na Kompyuta Mashuleni kwa bei nafuu sana


 

Kampuni yenye uzoefu katika ujenzi wa madarasa, maabara, majengo na uuzaji wa vifaa vya maabara ya masomo ya sayansi shuleni imeamua kuuza vifaa vya kuboresha elimu ya sayansi kwa bei ya kawaida na kuwezesha shule na vyuo kupata vifaa kwa wingi na vinavyokidhi ufundishaji, pia kompyuta zitauzwa kwa bei inayoridhisha ili kusadia kufundisha kwa kutumia video pasina mwalimu katika shule za vijijini na mijini. Hii ni rahisi kwa sasa kwani shule za vijijini nyingi sasa ni rahisi kupata umeme.

Kutokana na walimu kuwa wachache na wengine kukataa mazingira ya vijijini ni muda muafaka kutumia computer zenye kuonyesha video na kutoa sauti mbadala kwa pasipokuwa na walimu wa kutosha.

Video za masomo ya Hesabu na Sayansi zinaadaliwa ili kukidhi mahitaji kwa kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne kwa awamu ya kwanza ya mpango huu.





No comments:

Post a Comment